Akizungumza katika hotuba yake fupi wilayani Chato wakati wa sherehe za makabidhiano ya nyumba 50 za watumishi wa afya kwa mikoa mitatu ya Kagera, Simiyu na Geita, rais Dr. John Pombe Magufuli, amesema kuwa kumekuwa na visingizio kwa wanaobeba ujauzito wakiwa shuleni kwamba wamebakwa, akisema kuwa hilo haliwezekani kila mtu kubakwa, kwani wengi wao wamekuwa wakishinda na kukesha kwenye starehe zisizo rafiki.
Amesema kuwa Tanzania na watanzania wake wanataka maendeleo hivyo lazima serikali isimamie namna bora ya kuwaletea maendeleo hayo, bila kujali itikadi wala dini ya mtu, kwa lengo la kufanikisha azma hiyo, na kwamba wafanyabiashara ya mazao wasitozwe kodi kwa mzigo usiozidi tani moja, akitoa mbinu kuwa wanaweza kupitisha chini ya tani moja mara kadhaa kwa siku moja na kufanikisha shughuli yao bila bugdha.
..............BONYEZA CHINI KUSIKILIZA...................
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment