Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Pombe Magufuli, amesema kuwa hawezi kusahu alikotoka kwa kueleza kuwa aliuza furu, maziwa na kuchunga ng'ombe, kama sehemu ya maisha yaliyomwezesha kufika alipo, hivyo hataki kusikia watanzania wanaendelea kutahabika kama alivyotahabika.
Serikali kupitia mfuko wa Mkapa
foundation, imepanga kuajiri watumishi
104 wa afya katika mikoa ya Kagera, Geita na Simiyu.
Mwakilishi wa taasisi hiyo
amemweleza rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwamba pamoja na kuwezesha
utaratibu wa watumishi hao, taasisi hiyo imejenga nyumba hamsini kwa gharamna
ya shilingi bilioni 2.5.
Amesema kuwa nyumba hizo
zitatumika kwa watumishi hao pamoja na wengine kwenye mikoa hiyo, zikiwa kwenye
halmashauri ya Chato, Bukombe, Biharamulo na Maswa na zipo kwenye vituo vya
afya 25.
Hatahivyo mfuko huo umeshajenga
nyumba katika mikoa ya kusini zenye gharama ya shilingi bilioni 26.5.
Sherehe za makabidhiano
zinaendelea wilayani Chato, na mgeni rasmi ni rais mstaafu wa awamu ya tatu
Benjamin Mkapa, na kuhudhuriwa na rais John Pombe Magufuli, balozi wa Japan,
waziri wa afya Ummy Mwalimu pamoja na wakuu wa mikoa ya Kagera, Simiyu na
Geita.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment