Ahadi hiyo ilikiukwa kwa kubadili kanuni
kupitia sheria ya mipango miji ya mwaka 2007 (11)(2) kwa kutowasilisha rasimu
rasimu ya mradi wa viwanja 5000 ili wajadili mpano huo ili wakubali au wakatae
kama sheria inavyoelekeza.
Josephat Kyamwangire mzaliwa wa Bukoba
mjini kata ya Kahoro, ni katibu wa walalamikaji waliotwaliwa viwanja elfu tano
vilivyopimwa manispaa ya Bukoba, kinyume na makubaliano yao na viongozi wa
halmashauri.
Katika upimaji huo wa viwanja wananchi
wa manispaa Bukoba waliahidiwa kulipwa eneo linalochukuliwa na serikali, ilhaliwakisalia
na kiwanja kimoja kama walivyoaidiwa na aliyekuwa meya wa manispaa hiyo Dr
Anatory Aman.
Hatahivyo wananchi hawa wamenyimwa fursa
yakumilikishwa viwanja katika maeneo yaoya awali baada ya manispaa kugawa
viwanja vyote bila kuwapatia sehemu kama sera sheria na miongozo ya ardhi
kupitia sera ya makazi 2000,kanuni ya ukadiriaji na ulipwaji wa fidia kupitia
tangazo la serikali namba 78 na 79 la 2001.
Moja ya eneo lilopimwa na halmashauri katika manispaa ya Bukoba kwenye kata ya Nyanga. |
Ripoti iliyotolewa na wizara ya adrhi mjini Dodoma 16 NOVEMBA, 2012, Migogoro kati ya Jamii za
Wakulima na Wafugaji, Migogoro kati ya Wanavijiji na Wawekezaji, Migororo ya
Mipaka baina ya Mamlaka mbalimbali, Migogoro ya Wamiliki zaidi ya mmoja kwenye
kiwanja kimoja, Uvamizi wa mashamba/viwanja, Migogoro ya Wananchi kutoridhika
na fidia inayolipwa wakati wa utwaaji ardí.
Katika ya
Wilaya 135 ni 86 to au asilimia 64% zilizo na Maafisa ardhi wateule. Hali hii
inamaanisha kwamba Halmashauri nyingine hazina watendaji hawa kabisa au
zinategemea walio katika Halmashauri jirani. Maafisa Ardhi 2 wamesimamishwa
kazi. Wilaya ambazo zina watendaji chini ya asilimia hamsini ni Tabora, 33%,
Mwanza Manispaa 43%; Katavi 33%; Lindi 33%.
Na Mwanaharakati.