Hali hiyo ya mgomo ilianza jumatatu kama vyombo mbalimbali
vilivyotangaza mapema kuhusiana na mgomo wa amani kwa walimu kutokana na madai
yao mbalimbali.
Nilipozungumza na baadhi ya wanafunzi, katika mkoa wa
Singida wamesema kuwa baadhi ya walimu wanaonekana shuleni, lakini
hawafundishi.
Katika shule ya msingi MSIGIRI wanafunzi wamepewa adhabu za
hapa na pale baada ya kubainika na makosa madogomadogo jambo ambalo wamesema
hawakutendewa haki kwani ni adhabu bila masomo.
Kinachoangaliwa hapa ni jitihada za serikali kuweka
maelewano mazuri, lakini hata hivyo shule zingine wanafundisha japo kwa
kujificha na jitihada za kupata walimu wa shule nilizopitia bado hazikuzaa
matunda.
No comments:
Post a Comment