MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 17 October 2012

Balozi KHAMIS SUED KAGASHEKI, amesema kuwa TANZANIA inaendelea kuboresha mpango wa Uhifadhi endelevu, kwa kuwa nchi inatambua manufaa yatokanayo na uhifadhi.

Waziri KAGASHEKI  ametoa kauli hiyo jijini ARUSHA,  wakati wa chakula cha jioni kwa Washiriki wa Kongamano la kwanza la Afrika,  kuhusu Usimamizi wa Utalii endelevu katika Hifadhi za Taifa.

Picha chini ikionyesha kikundi cha ngoma  cha arusha kikitumbuiza katika hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na wizara ya maliasili na utalii(picha na mahmoud ahmad)
Katika kongamano hilo,  ambalo limehusisha Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani –UN  WTO- pamoja na Mawaziri wenye dhamana ya Mazingira na Utalii kutoka nchi  mbali mbali,  Waziri KAGASHEKI  amesema asilimia 24 ya Wizara ya Maliasili imetengwa kwa ajili ya kuendeleza uhifadhi.

Amesema TANZANIA imejifunza na kufaidika na mambo mengi,  kutokana na kuwa Mwanachama wa UN  WTO,  tangu ijiunge na Shirikisho hilo mwaka 1975.

Kwa upande wake,  Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani,  Dk TALEB   RIFAI,  ameziasa nchi za Afrika kuendeleza hifadhi,  ili ziwe endelevu kuchangia katika kukuza  Utalii bila kuwa na madhara.

No comments: