MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday 17 December 2012

LOWASA KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA KANISA

Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amesisitizia tena kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni jambo la hatari kwa usalama wa nchi,wakati alipokuwa katika harambee ya kuchangia ukarabati wa kanisa la kilutheri usharika wa Akyeri Meru mkoani Arusha, Mh lowassa ameonya kuwa suala hilo lisiposhughulikiwa haraka litasababisha hali ya hatari.
Amesema kuwa tunashuhudia maandamano katika mataifa ya ulaya vijana wakidai hali bora ya maisha pamoja na ajira.hali hiyo tusipoangalia inaweza kutokea hapa nchini kwetu.

huko nyuma niliwahi kusema kuwa makanisa, mashirika na watu binafsi wasaidie juhudi za serikali kutatua suala hilo''alisema Lowassa.

Lowassa ambaye katika harambee hiyo aliongozana na marafiki zake, ambapo yeye na familia yake pamoja na marafiki zake wamechangia kiasi cha shilingi millioni 33.2.


Zaidi ya shilingi millioni 160 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana katika harambee hiyo.

Kwa upande wake askofu Akyoo wa jimbo la Meru alimsifu Lowassa kwa uchapakazi wake popote alipokuwa.''Wakati ulipokuwa Waziri Mkuu ukimsaidia rais tulishuhudia uwezo wako mkubwa katika kufuatilia majukumu yako''alisema na kuongeza kuwa Lowassa ni mtu wa ibada

No comments: