MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 3 December 2012

MKURUGENZI MANISPAA YA BUKOBA AKILI KUTOKUWAPO KWA MKATABA WA UJENZI WA SOKO JIPYA LA BUKOBA

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kagera katika ukumbi wa manispaa ya Bukoba, mkurugenzi huyo Bwana HAMIS KAPUTA, amesema halmashauri hiyi haijaingia mkataba wowote kuhusu ujenzi wa soko kutokana na kutofanyika kwa upembuzi yakinifu kuhusu soko hilo.

Hata hivyo amesema kuwa kuna kesi ya wafanyabiashara wa soko hilo ambao waliifungua wakidai kulipwa fidia ya bilioni tano kutokana na kutoshirikishwa katia suala la kuvunja soko hilo.

Amesema kuwa kesi inatakiwa kusikilizwa mwezi machi mwaka ujao hivyo ni vugumu utekelezaji wa ujenzi wa soko kufanyika wakati huu ambapo ameshindwa kuthibitisha ni lini soko litavunjwa kwasababu hali hiyo itakuja baada ya hukumu ya kesi iliyoko mahakamani.

Ni baada ya zaidi ya wiki moja baada ya mbunge wa Bukoba mjini kusema kuwa kama taratibu sahihi hazifanyiki hakuna kuvunja soko hilo huku akisema kuwa hakuna panapofanyika uvunjaji bila kufuata taratibu sahihi.

No comments: