Waziri wa ardhi nyumba na makazi Profesa Anna Tibaijuka, ameitaka ofisi ya ushuru
wa forodha mkoa wa Kagera, kuhakikisha inaweka mipango mizuri katika kituo cha
mtukula ili kupunguza usumbufu wa watumiaji
wa mpaka huo.
Akizungumza na ofisa fordha wa kituo cha mtukula bwana PANGANI, Profesa
Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuondoa
usumbufu, mkoa utajipatia faida baada ya kufanya shughuli zake kwa haraka.
Ametoa kauli hiyo baada ya kuona mpaka wa mtukula
umejaa magari makubwa ambayo yantoka
nchini Uganda, na kusababisha foleni kubwa ambayo hata hivyo inaingiza kiasi
kidgogo cha fedha kwani magari hayo yanatozwa shilingi 3000/= tu kwa siku.
Ameongeza kuwa kiasi cha ushuru kikiwa kikubwa
usumbufu utapungua.
Kwa upande wake afisa forodha wa kituo cha mtukula
bwana PRIMUS PANGANI, amesema kuwa magari hayo yanalipiwa shilingi elfu 3, na
kuwa taratibu zote zinakuwa zimekamilishwa kwa upande wa Tanzania, isipokuwa
waganda wanakuwa hawajakamilisha ndiyo maana yanaendelea kuwepo.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment