Baada ya kufika eneo hilo walishangaa kuona wanavamiwa na kupigwa na kufungiwa kwenye kibanda wanachokiita sero ya wanamgambo kilichopo katika uwanja wa kataiba huku wakimwagiwa maji na kulazimishwa kukaa kwenye sementi ambapo walipigwa na mwanamke ambaye jina linahifadhiwa alitenguliwa mkono.
Nimejitahidi kumtafuta mkurugenzi manispaa HAMIS KAPUTA ila ushirikiano wake katika hilo haukupatikana, japo mtendaji wa kata Kagondo naye amesema kuwa hajui kwanini walifanyiwa hivyo kwasababu wakati wanaingia eneo hilo yeye hakupewa taarifa.
Wananchi wanasema wanalima katika eneo hilo, baada ya kuonekana kuna majengo ya viongozi kama Meya wa manispaa amejenga hapo, na mtendaji wa kata amejenga kwenye eneo hilo, jambo ambalo linawapa wasiwasi kwanini wao waambiwe kuwa wafuate amri ya mkuu wa mkoa ya kusafisha mazingira na kutunza vyanzo vya maji wakati viongozi hawatekelezi hilo?
Ni mwezi sasa tangu mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu FABIEN MASSAWE, kumtaka mkirugenzi manispaa ahakikishe anawaondoa wale wote waliojenga na kuendelea kufanya shughuli kwenye maeneo tengefu.
MWANA HARAKATI
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment