MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday 18 March 2013

PROFESA ANNA TIBAIJUKA; WANANCHI WAPIMIWE ARDHI NAKUPEWA HATI ZA UMILIKI

 
 Amekemea tabia ya halmashauri kutumia fedha za wataalamu wa ardhi na wizara ya ardhi, kwani zipo na zinatolewa ili kufanya shughuli za kitaalamu kwa kuwapimia na kuwatengea maeneo pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.

 Waziri Tibaijuka amesema kuwa wamefanya mazungumzo na waziri wa maliasili na utalii Balozi Hamis Kagasheki, na kukubalia kutenga eneo kwa ajili ya wafugaji wa ndani ya nchi, kwani wameonekana kunyanyaswa na wasimamizi wa ardhi mkoani Kagera hasa maeneo ya Karagwe, Bihalamuro na Muleba, huku wakionekana kuwakumbatia wanyarwanda.

Kwasasa manispaa ya Bukoba imepima zaidi ya viwanja 4800, na imefidia wananchi kadhaa, jambo ambalo Prof amelitilia shaka na akauliza swali kama Kigambo fidia kwa ekali moja ni milion141 kwa manispaa ni sh ngapi?

No comments: