Lakini tume ya uchaguzi itakagua
hesabu hiyo kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada
yawakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu na
kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya
uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila
Odinga akipata 5,340,546
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka
katika mahakama ya kimataifa ya ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi
mkuu wa mwaka wa 2007.
Waandishi wa BBC wanasema iwapo
Kenyatta atakabidhiwa ushindi katika raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri
Mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Tume ya uchaguzi itatangaza matokeo
rasmi ya mshindi baadaye leo
Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa
uchaguzi huo na vile vile kama mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya
kutangazwa kuwa rais wa nne wa Kenya.
Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa
hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume Isaack Hassan.
Vile vile mgombea huyo pia lazima
awe ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga
alikuwa amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili
azungumzie maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo uliakhirishwa
hadi siku ya Jumamosi , baada ya tume ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho.
No comments:
Post a Comment