Diwani wa kata
ya mpunguzi mh john Matonya ameseama pamoja na idadi hiyo ya nyumba
zilizo anguka bado nyingine zinaendelea kuanguka .
Aidha mh matonya amesema miundombinu mibovu
ndio chanzo cha mafuriko hayo kutokana na kujengwa bila kiwango kizuri.
Hata hivyo mh matonya ameomba miundombinu
iboreshwe ili kuondoa adha ya mafuriko wakati mvua zinaponyesha.
WAMILIKI WA MITANDAO YA SIMU ZA
MKONONI TANZANIA WAMEELEZA SABABU ZINAZOPELEKEA WAO
KUSHINDWA KUWEKA MINARA YA SIMU KATIKA MAENEO YA
VIJIJINI
Hayo yamejiri mara baada ya wakazi wa
kijiji cha solowu wilayani chamwino kulalamikia ukosefu wa
mawasiliano ya mitandao ya simu kwa muda mrefu .
Mfanyakazi wa mtandao wa zantel Bw Brayan Donard
amesema ukosefu wa miundombinu vijijini ndo sababu
kubwa inayowapelekea wao kushindwa kuwafikia wakazi
wa maeneo hayo.
Aidha Bwana Brayani ameongezea kuwa
wana malengo ya kuwafika watanzania wote ila kwa sasa wameanza na wakazi wa
Dodoma mjini na wanaelekea vijijini.
Sanjari na hayo amewataka
wakazi wa maeneo ambayo yamekuwa yana matatizo ya
mtandao wawe wavumilivu kwani wanawakumbuka na muda
ukifika watawafikia
DIWANI WA KATA YA CHILONWA WILAYANI
CHAMWINO AMEITAKA SERIKALI KUJENGA DARAJA LA CHILONWA LILILOSABABISHA
WATU WATATU KUPOTEZA MAISHA KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.
Mh Yaledi
Sinon amesema tangu kutokea kwa tukio hilo mpaka sasa hakuna harakati
zinazofanyika baada ya meneja wa mkoa kuahidi kutafuta jitihada za matengenezo.
Aidha mh Sinoni amesema tangu kutokea
tukio hilo mpaka hivi sasa hakuna kiongozi yeyote aliefika hapo kwa
ajili ya kutatua kero hiyo.
Hata hivyo ameomba madereva kuwa makini
katika daraja hilo kutokana na kuendelea kunyesha kwa mvua na kuwataka
makandarasi kutengeneza daraja hilo.
ZAIDI YA MAGARI 1,000 YAMEKWAMA KWENYE
BARABARA KUU YA MWANZA KWENDA DAR ES SALAAM KATIKA KATA YA MIGUWA,
WILAYANI NZEGA, KUTOKANA UTEKAJI WA MALORI ULIOFANYWA HIVI KARIBUNI.
Madereva wamegoma kuondoa magari yao baada
ya kukasirishwa na kitendo cha polisi wa Nzega kushindwa kuwasaidia wakati
walipotekwa.
Kutokana na tukio hilo,madereva wamegoma
kuondoa magari yao na kusababisha mabasi ya abiria na malori ya mizigo kukwama
wakati abiria wapatao 3,000 wakitaabika kwa kukosa chakula na maji.
Aidha Madereva hao wameapa kutoondoa magari
hayo hadi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe
na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa watakapofika kwenye eneo hilo ili
kusikiliza kilio chao.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya
ya Nzega, Emmanuel Mihayo amesema watu wamejeruhiwa vibaya kwenye utekaji huo
kwa kukatwa masikio na kutobolewa macho.
WATU WANNE WAMEPOTEZA MAISHA KWA KUSOMBWA
NA MAJI MKOANI HAPA , KUTOKANA NA MVUA ZINAZO ENDELEA KUNYESHA NCHINI.
Katika tukio la hivi karibuni mkazi
mmoja wa kijiji cha Mpinga mwenye umri wa miaka 55 amefariki baada ya
kutumbukia kwenye mto Mpinga ambao ni wa msimu.
Kamanda Misime amesema tukio jingine
limetokea mwanzoni mwa wiki iliyopita, ambapo watu wanne
walitumbukia na gari waliyokuwa wakisafiria katika mto Chinyasungwi,
kijiji cha Mahampa, Wilayani Chamwino na watatu kati yao walikufa huku
mmoja akiokolewa.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment