Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi
cha Komando kuanza ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ
Mkoani Morogoro.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea
taarifa ya Utawala na Utendaji kivita kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Komando
wakati wa ziara yake.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa
maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea
katika kikosi cha Komando.
Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani lililojengwa
kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea kusaidia usafirishaji wa
zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile.
=Akizungumza katika kikao maalum na
Maafisa Askari wa vikosi hivyo,Rais Kikwete amesema ameridhishwa sana na
utimamu wa vikosi hivyo kimafunzo na pia amehidi kukiongezea vifaa zaidi kikosi
cha Uhandisi wa Medani ili kiweze kupambana na majanga hapa nchini.
Rais Kikwete pia amelitaka Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kubuni mikakati ya kuondokana na Makazi ya muda.
Katika Kikao hicho,Rais Kikwete aliligusia swala ta tatizo la Maji linalovikabili vikosi hivyo,ambapo ameahidi kulishungulikia ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2014.
Katika Kikao hicho,Rais Kikwete aliligusia swala ta tatizo la Maji linalovikabili vikosi hivyo,ambapo ameahidi kulishungulikia ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2014.
Katika ziara hiyo,Rais aliambatana
pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi,
Makamishna Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na
Mkoa wa Morogoro.
Picha/habari na Luteni Kanali Juma
Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment