MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 4 March 2014

WAZEE HATARINI BUKOBA

 Ni katika ukosefu wa vyoo, tiba, na kulala mchanganyiko wanaume kwa wanawake, kwenye kituo cha wazee cha Kiilima Bukoba vijijini mkoani Kagera.
 Kituo hicho kinalea jumla ya watu 24, wazee 13,watoto 11, ambapo wazee wanaume ni 7 na wanawake 6, ambapo miongoni mwa wanawake hao wapo wanaobebeshwa mimba na kujifungua watoto ndiyo maana kunakuwapo na watoto pia kituoni hapo.
 Picha juu ni bibi mwenye umri wa miaka zaidi 100, na chini ni mzee akisubara mara baada ya kukosa huduma ya choo karibu na hatahivyo choo kilichopo ni cha ajabu.
Picha chini ndiyo maisha halisi ya wazee hawa kila siku ya Mungu na hapa wamepunmuzika.


 Chini ni miongoni mwa wazee wasioona, akinieleza jinsi anavyolala kwa tabu kutokana na ugonjwa uliokuwa unamsumbua wa kujikuna lakini hatahivyo anasema kwa sasa hali ni afadhari, picha juu ndiyo mazingira halisi ya wazee hao wanavyoshinda kila kukicha.

 Picha juu ni mwenyekiti wa wazee hao ambaye yeye anaugonjwa wa ukoma pamoja na uzee wake, hana vidole vya mikono wala miguu lakini ametaja kero zinazowakabili kuwa ni ukosefu wa tiba halisi na kushindwa kutibiwa wanapofikishwa hospitalini huku wakitelekezwa wakati wanaambiwa kuwa huduma kwa wazee ni  bure.
 Juu na chini ni vyoo viwili tofauti wanavyotumia wazee hawa vikionesha kutokuwa na kiwango chochote kwao kukidhi aja ambapo hapo juu ni choo cha banzi hatahivyo wazee wengine hawaoni hivyo inakuwa shida kwao kukitumia, na chini hapo hakuna uzio wowote  hivyo mzee akiwa anajisaidia anayebahatika kufika hapo lazima achunguliwe.

 Picha juu ni choo kinachojengwa ambacho hatahivyo kimechukua muda mrefu kukamilika ambapo kinasimamiwa na mtu binafsi, kwa msaada wa mashirika ya nje, chini ni mlemavu wa viungo ambaye ni miongoni mwa wazee akizungumza nami, lakini kubwa zaidi kwake anaomba msaada wa elfu 50 ili ajenge banda la kuku kwani yeye upendelea kulima na kufugana, katika kujisaidia amesema kuwa anatumia akili ya kuzaliwa hivyo hatumii vyoo wanavyotumia wengine.
 Chini niliamua kufanya mazungumzo na msimamizi wa kituo hicho ambaye pamoja na mambo mengine, amaesema wana kero nyingi ikiwamo ukosefu wa huduma ya usafiri, umeme, maji na kukabiliwa na baadhi ya wazee wenye upungufu wa akili wanaosababisha usumbufu mkubwa ilihali huduma ya matibabu kwa wazee ikiwa kero kubwa.

Chini ni jengo ambalo lilikuwa likitumika awali kama moja ya bweni na ndilo jinsi moja ilitumia, lakini liliezuliwa na upepo miaka2 iliyopita na mkuu wa mkoa wa Kagera Fabian Massawe alifika na kuahidi kulikarabati lakini hadi sasa bado ndiyo maana wazee hao wanalala mchanganyiko.
                                      
                                                   
                                      
 Juu nijiko linalotumiwa kuwapikia wazee chakula.
 Picha juu ikiwa ni moja ya kitanda wanavyolalaia wazee hao, chini ni mimi nikifanya mazungumzo na mchungaji anayesimamia miradi ya kituo hicho kama ujenzi wa choo, shamba lenye ekari 30 ambalo lipo katika hatua ya kwanza ya kutifuliwa kwa Trekta, hapo tunatoka kukagua shamba lenyewe.

Chini ni jembe linalotumika kama kengele wapigiwayo wazee kuwakusanya lakini mlezi amesema kuwa kengele iliyokuwapo iliibiwa wakaamua kutundika jenmbe kwenye mwembe.

Fuatilia kipindi cha redio 88.5MHz kusikiliza mboni ya jicho kila Ijumaa sa3:15 usiku na marudio jumapili saa1:00 jioni.
MWANA HARAKATI

No comments: