MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 6 April 2014

MAAJABU!!! MGANGA WA JADI AMSABABISHIA MADHARA MTEJA BAADA YA KUNG'ATWA SEHEMU ZA SIRI NA MBWA MWITU

Kijana Chamangeni Zulu wa Malawi, ameng’atwa sehemu zake za siri na fisi pamoja na kukatwa vidole vitatu.
Chamangeni akiwa hospitalini.
Zulu alitaka utajiri na akaenda kwa mganga ambaye alimweleza kuwa ili aweze kuwa tajiri anatakiwa kupoteza sehemu ya viungo vya mwili wake.

Kwa sasa Zulu yupo kwenye hospitali Kuu ya Chipata nchini Zambia karibu na mpaka wa Malawi, baada ya mwenyewe fisi amle sehemu zake za siri.

Zulu ameliambia gazeti la The Times kuwa "Nilikutana na wafanyabiashara walionieleza kuwa njia nzuri ya kuwa tajiri ni kutoa sehemu ya viungo vyangu vya mwili".

Anasema majira ya saa 10 alfajiri wiki mbili zilizopita alikwenda msituni kwa upande wa Zambia.

"Nilielekezwa niwe uchi na nilipofika huko alikuja fisi akaanza kunila vidole vyangu na mara akala sehemu zangu za siri,"anasimulia.
Zulu anasema mganga aliyempa maelekezo hayo hakumweleza wazi kuwa sehemu zake za siri zitapotea zote.

Licha ya tukio hilo la kumuumiza, Zulu anaamini atakuwa tajiri baada ya nyeti zake kuliwa.

"Hata kama nimepoteza sehemu muhimu za mwili wangu bado naamini nitakuwa tajiri,"anasema.

Uongozi wa Hospitali ya Chipata umesema Zulu alifikishwa hospitalini hapo na maofisa polisi na hali yake inaendelea vizuri. 

Mwaka 2012 umbali wa maili 50 katika eneo la Chadiza mwanaume mmoja alivamiwa na mnyama wakati akienda kujisaidia kwenye bustani yake.

Mwanaume huyo, Isaac Mwale(42) alisema alimuona mnyama mweusi anayefanana na mbwa na kumvamia kabla ya klumtaka mguu na kuondoka nao.

Baada ya shambulio hilo, wanakijiji walishitaki kwenye Mamlaka ya Wanyamapori ya Zambia kupunguza idadi ya fisi katika eneo hilo.
Na Mwanaharakati.

No comments: