
Watoto hao pia walikuwa wanapumua
bila usaidizi wowote walipotolewa kutoka katika mashine yenye hewa ya Oxygen.
Mama wa watoto hao, alisema kuwa
watoto hao waliopewa majina ya Jillian na Jenna Thistlewaite walikuwa
wameshikana katika kitovu na kutumia Kondo moja la nyuma , hali ambayo
madaktari walisema ni nadra.
"Tayari wanaonekana kuwa
marafiki ,’’ alisema mama yao Sarah Thistlethwaite.
Walizaliwa Ijumaa katika jimbo la
Ohio, wakiwa wameshikana mikono.
Inaarifiwa ni mama mmoja tu kati ya
akina mama elfu kumi mwenye uwezo wa kujifungua watoto pacha wa aina hiyo.
Bi Thistlewaite, mwenye umri wa miaka
32,alilazimika kupumzika kwa wiki kadhaa kabla ya kujifungua kwani pacha
wanaozaliwa wakiwa wameshikana mikoni ni hali nadra ambayo inaweza kuhatarisha
maisha ya watoto na mama kabla ya kuzaliwa.
Mama huyo alisema kupokea watoto
wake ilikuwa zawadi tosha kwake wakati huu wa kusherehekea siku ya akina mama
duniani.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment