Kwa mujibu wa mrembo huyo, Lulu
Jumanne ‘Selina’, alifahamiana na marehemu Kuambiana mwaka 2006 akamwambia ndoa
yake haipo sawasawa.
Alisema walianzisha uhusiano lakini
haukuwa wazi katika jamii. Alisema siku moja akiwa anaishi Mwananyamala, wazazi
wake walimtembelea.
“Nikiwa na wazazi nilimwona
Kuambiana anapiga hodi, akaingia akiwa na begi la nguo. Niliogopa kwani
wazazi walikuwepo na walikuwa hawamtambui.
“Hata hivyo, walielewa yakapita,
tukawa tunaishi wote nyumbani kwa kupika na kupakua,” alisema Selina ambaye
naye ni mwigizaji.
Aliendelea kuweka wazi kwamba, baada
ya hapo maisha yaliendelea lakini ikafika mahali marehemu akahamishia mapenzi
kwa Mbongo Fleva, Stara Thomas yeye akawa ‘zilipendwa’.
Akizidi kuanika mambo kuwa mwaka jana Kuambiana alirudi kwake baada ya kutofautiana na Stara, akataka waendelee na mapenzi yao.
Katika mahojiano mafupi kati ya
Selina na gazeti hili, mambo yalikuwa hivi:
Ijumaa: Mlikuwa na mipango gani ya maisha?
Selina: Mingi tu. Kwanza
alishanitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake na wadogo zake.
Ijumaa: Marehemu alionesha upendo wa dhati kwako?
Ijumaa: Marehemu alionesha upendo wa dhati kwako?
Selina: Sana tu, kwani alipenda
kuniita mke wake. Alikuwa ananiheshimu hadi mwisho. Hakuwa akipenda mwanaume
anizoee.
Ijumaa: Unajua nini kuhusu kuumwa kwake?
Selina: Najua alikuwa anaumwa tumbo kwa muda mrefu. Alikuwa akila chakula cha maelekezo ya daktari.
Ijumaa: Unajua nini kuhusu kuumwa kwake?
Selina: Najua alikuwa anaumwa tumbo kwa muda mrefu. Alikuwa akila chakula cha maelekezo ya daktari.
Ijumaa: Mara ya mwisho ulizungumza
naye nini?
Selina: Nilimshauri anunue simu yenye WhatsApp kwani mara nyingi Kuambiana alikuwa hapatikani hewani. Alikuwa hawezi kukaa na simu kwa muda mrefu.
Selina: Nilimshauri anunue simu yenye WhatsApp kwani mara nyingi Kuambiana alikuwa hapatikani hewani. Alikuwa hawezi kukaa na simu kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Selina alisema hapendi
kueleza mengi lakini anaamini yeye ndiye mwanamke wa mwisho katika mapenzi na
marehemu.
Na GAZETI LA IJUMAA
No comments:
Post a Comment