
Akizungumza kwenye Kanisa la Imani Makongoro Misheni jana,
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria, Andrew Gulle alisema
wanaamini shambulio hilo ni la kigaidi na kwamba, Serikali inapaswa kuchukua
hatua ya kuwasaka wanaohusika.
“Kanisa tunaamini tukio hili linahusiana na ugaidi, umefika
wakati Serikali ikachukua hatua za kuwasaka waliohusika ili sheria ifuate
mkondo wake,” alisema Gulle.
Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya dini wanasema huenda
tukio hilo linatokana na migogoro inayoendelea kanisani hapo kwa sababu tayari
kuna baadhi ya waumini wamejitenga kwa kuanzisha kanisa lingine.
“Wasikwepe matatizo yao ya ndani, kuna askofu aliuawa kwa
kupigwa tofali kutokana na migogoro, hivyo hata hili (tukio) litakuwa ni
migogoro inayoendelea,” alisema mmoja wa waumini ambaye hakutaka kutajwa jina
lake.
Askofu Gulle alikanusha kuwapo kwa migogoro kanisani hapo na
kwamba, tukio hilo halihusiani na mgogoro wowote ndani ya Kanisa bali ni
ugaidi.
Hali ya majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea kanisani hapo,
Benadeta Alfred, imeelezwa kuendelea vizuri katika Hospitali ya Rufaa ya
Bugando alikolazwa. “Hali ya mgonjwa ni nzuri ukilinganisha na tulivyompokea
kwani hata kuongea alikuwa hawezi, lakini hivi sasa anaweza kuongea japo kwa
shida,” alisema Lema.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment