TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 5/ 2014
MTAALAMU WA NYASI BANDIA AWASILI
Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClemen amewasili nchini
leo alfajiri (Mei 4 mwaka huu) ambapo atakuwepo kwa siku tatu.
![]() |
| McClemen, akiwa Bukoba |
McClemen ameondoka leo (Mei 4 mwak
huu) kwenda Bukoba ambapo atakagua Uwanja wa Kaitaba, na kesho (Mei 5 mwaka
huu) atakwenda jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.
Viwanja hivyo vinawekwa nyasi bandia
kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya
ukaguzi huo, McClemen atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze
kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa
nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es
Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU
TANZANIA (TFF)
Na Mwanaharakati.



No comments:
Post a Comment