Kauli hiyo imetolewa na
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alipokuwa akitoa hotuba yake kwa Magavana wa
nchi za Afrika katika mkutano wa mwaka wa wadau wa Benki ya Afrika jijini
Kigali, Rwanda.
Mh.Saada amesema kuwa
kupitia mpango wa GCI-VI Tanzania imekuwa na uwezo wa kulipa hisa zake zipatazo
Dola za Kimarekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda uliopangwa.
Saada amesema kuwa
kupitia mpango wa GCI-VI Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kulipa hisa
zake zipatazo Dola za Kimarekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda
uliopangwa.
Zaidi ya hayo, Waziri
Saada ameendelea kusema kuwa nchi yake imeweza kulipa hisa zake za awamu ya nne
zipatazo kiasi cha Dola za Kimareka 1,279.30 kabala ya muda uliopangwa.
“Ninaamini ni katika
mkutano huu tunaweza kujadili dira ya Benki katika miaka mingine 50 ijayo kama
kauli mbiu ya mkutano huu inavyothibitisha, “Afrika tunayoitaka miaka 50 ijayo”
alisema Waziri Saada.
Aidha, Waziri Saada
alimpongeza Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Donald Kaberuka na
uongozi mzima kwa kusimamia na kuongoza kwa umahiri mkubwa majukumu walionayo
ya kibenki na kuhakikisha inasonga mbele daima na kuifanya kuwa benki bora
barani humu.
Ili kuhakikisha malengo
hayo yanafikiwa bara hili lazima kudumisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali
za kijamii na kujipatia maendeleo endelevu kwa nchi zao na watu wake. Mwaka huu
Benki ya Afrika inafikisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwake ambapo imeendelea
kuhudumia bara hili kwa mafanikio makubwa.
Kwa upande wake
Rais wa Rwanda Paul Kagame akifungua mkutano huo alisema kuwa ili kufikia
uchumi wa kati katika Bara la Afrika kwa miaka 50 ijayo inabidi nguvu
kubwa ielekezwe kwenye sekta binafsi ambayo itatengeneza ajira kwa vijana na
wanawake.
Mkutano huo ni wa
siku tano kuanzia 19 hadi 23 Mei mwaka huu ambapo kabla ya ufunguzi wa
Mkutano huu ulitanguliwa na mikutano mbalimbali ya Magavana ambao ni Mawaziri
wa Fedha kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiambatana na wajumbe
kuwakilisha nchi zao.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment