MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 18 May 2014

SHULE ZA MSINGI DODOMA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO

Wakazi wa mkoa wa Dodoma wametakiwa  kutoa ushirikiano katika masuala ya Elimu ili kutatua changamoto ya miundombinu inayo zikabili shule nyingi kwa sasa. 

Akizungumza na mtandao huu, afisa elimu wa mkoa wa Dodoma mwalimu Juma Kaponda amesema serikali inaendelea kutoa fedha katika shule mbalimbali lakini bado kunachangamoto kubwa ya vyumba vya madarasa pamoja  na madawati.

Aidha mwalimu Kaponda  amesema serikali kwa kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa(BRN) imeanza kuleta maendeleo mazuri  japo bado kuna changamoto za upungufu wa madawati ambapo amewataka wananchi kushirikiana na serikali ili kuondo changamoto hizo.

Sanjari na hayo amesema  kwa sasa mkoa wa Dodoma umejipanga vizuri ili kutoa mfunzo kwa walimu na  kupata walimu bora kwaajili  ya shule za sekondari pamoja na shule za msingi
Na Mwanaharakati.

No comments: