Umoja wa Afrika (UA) (kiingereza:
African Union (AU); kifaransa: Union africaine (UA); Kihispania:
Unión Africana (UA) ; Kireno: União Africana (UA) ) ni muungano wa nchi 54 za
Afrika
ulioanzishwa Julai 2002. Umoja huu unaendeleza kazi za Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa
kiingereza: Organisation of African Union - OAU).
![]() |
Ramani ya afrika kuonesha nchi zote za umoja huo ispokuwa Moroko. |
![]() |
Bendera ya AU |
Nia ya umoja huu ni kujenga muundo na
mfumo wa kisiasa, kiuchumi, na kijamii ili kufikia wakati ambapo bara la Afrika
litakuwa na bunge moja, benki moja, jeshi moja, rais mmoja, sarafu moja, n.k.
Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuungannisha nguvu za mataifa ya Afrika ili
kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile vita, njaa, ukimwi,
n.k.
Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika ulifanyika mwaka 2004 huko Afrika Kusini, na mfululizo wa mikutano hiyo ni kama ifuatavyo;-
1.
Durban (Afrika Kusini): 9-11 Jul.
2002.
2.
Maputo (Msumbiji): 10-11 Jul. 2003.
3.
Sirte (Libya), mkutano wa dharura:
Feb. 2004.
4.
Addis Ababa (Ethiopia): 6-8 Jul.
2004.
5.
Abuja (Nigeria): 24-31 Jan. 2005.
6.
Sirte (Libya): 28 Jun. - 5 Jul.
2005.
7.
Khartoum (Sudan): 16-24 Jan. 2006.
Mwenyekiti wa UA hivi sasa Denis Sassou-Nguesso na
Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya UA ni Alpha Oumar Konaré. Spika
wa Bunge la Umoja wa Afrika ni Getrude
Mongella.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment