MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 15 June 2014

MWANAFUNZI ALISHWA KINYESI CHAKE GEITA


MWANAFUNZI wa miaka 8 Rachel Isaya wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Nyakabale wilayani Geita, amelishwa kinyesi chake baada ya kukutwa anajisaidia kwenye kisima akiwa na wenzake wakitoka shuleni.

Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa tukio hili limetokea tarehe 11 mwezi huu majira ya saa 4 asubuhi wanafunzi hao walipokuwa wanatoka shuleni kufanya usafi  mwanafunzi huyo akiwa na wenzake watatu ambao hawakufahamika majina yao  walipofika eneo hilo Rachel alienda kujisaidia karibu na kisima hicho cha  Marco Maico.

Konyo ameendelea kusema kuwa mara tu alipomaliza kujisaidia Marco alipita na kukuta kinyesi hicho ambapo alimwamuru akizoe kwa mkono kinyesi hcho hata hivyo alipoenda kukitupa Marco akamwambia akile hadi kiishe na kwa hofu ya kutaka kupigwa alikila kinyesi hicho huku wenzake wakimsubili baada ya kumaliza alienda nyumbani na wenzake.

Baada ya kufika nyumbani mwanafunzi huyo alimwambia mama yake Agnes Lujaja(26) juu ya kilichotokea na mama yake akaenda kwa balozi wa nyumba kumi kutoa taarifa ambapo akampa barua ya kumpeleka zahanati ya Nyakabale kwa matibabu zaidi baadaye balozi huyo alitoa taarifa kwa Polisi na baada ya mda walifika kwenye eneo la tukio na kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo.

Katika hatua  nyingine kamanda Konyo amesema kuwa Jumanne Joel(25-30) ameuawa na wananchi wenye hasira kali mara baada ya kumvamia Monica Lutonja(32)  wa kijiji cha nyankumbu katika kata ya kalangalala mjini hapa .

Aidha tukio hilo limetokea usiku nwa kuamkia leo ambapo inadaiwa kuwa watu watatu akiwemo marehemu walienda kwa mama huyo na kugonga hodi wakidai kuwa wao na rafiki wa kaka yake ambaye ni Bunegezi na alipofungua walianza kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kupoteza fahamu.

Hata hivyo kelele za mama huyo zilisababisha majirani kutoka na kuanza kuwasaka baada ya kuwa wamekimbia na hatimaye wakamkamata mmoja na wakaanza kumpiga hadi kumuua.

Kamanda amesema kuwa watuhumiwa wengine wawili bado wanatafutwa na jeshi la polisi kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Na Mwanaharakati.

No comments: