Tukio hilo ambalo kamwe Luca hawezi
kulisahahu maishani mwake, lilijiri kwenye gesti hiyo iliyopo karibu na Kituo
Kikuu cha Mabasi cha Segerea, Dar, Jumanne iliyopita huku mzee huyo akishushiwa
tuhuma nzito ya rushwa ya ngono kwa vibinti chini ya miaka 18.
Katika tukio hilo, mzee huyo wa
kanisa na msanii huyo wa Kundi la Maigizo la Vivif lenye maskani yake maeneo
hayo walikuwa wamejichimbia kwenye gesti hiyo katika chumba ambacho mlangoni
kilikuwa kimeandikwa Rombo kabla ya kuchomolewa na kufikishwa kanisani kisha
polisi.
Fumanizi hilo lilikuwa
limesukwa na wasanii wa kundi hilo
kwa lengo la kumkomoa mzee huyo wa
kanisa ambaye alikuwa ni mfadhili wa kundi lao aliyeanza
kutumia mgongo wa ufadhili kuwatongoza
mabinti wa kundi hilo mmoja baada ya
mwingine.
Wakiwa ndani ya
gesti hiyo, wasanii wa kundi hilo walivamia
chumba hicho na kuanza kumchomoa mzee
huyo ambaye aliruka ukuta na kudondokea kwenye matuta ya
viazi.
Akiwa anajizoazoa kwenye matuta
hayo, kundi la wasanii hao lilimuunganishia ambapo kabla ya kumnasa aliingia
kwenye chumba cha nyumba iliyopo jirani na gesti hiyo ili kujisalimisha.
Hata hivyo, zoezi lake lilifeli
baada ya wasanii hao kumtahadhalisha mwenye nyumba hiyo kuwa wanamtaka
mtuhumiwa wao la sivyo wangeichoma moto.
Baada ya kuzingirwa na wasanii hao
huku akihatarisha maisha yake kwa kuwa wasanii hao walikuwa na hasira, aliona
yasiwe makuu akaamua kuwaruhusu wamtoe mtuhumiwa wao wakamalizane naye
kanisani.
Alipotiwa mikononi, mzee huyo wa
kanisa aliomba apelekwe kanisani ambapo hapakuwa mbali na eneo la tukio ili
akahifadhi vitu vyake muhimu pamoja na kuomba ushauri.
Kundi hilo la wasanii lilimpeleka
kanisani msobemsobe ambapo baada ya hatua kadhaa polisi walitokea na
kuwadhibiti wananchi wenye hasira na wasanii waliotaka kumdhuru mzee huyo wa
kanisa wakati akipelekwa kanisani.
Wakiwa mitaani, njiani mabinti
walikuwa wakipiga kelele ‘weraaa…ukomeee…’ huku wakifurahia kufunga mitaa kwa
madai kwamba mzee huyo wa kanisa alizidi.
Katika sekeseke hilo, polisi hao
walimtia pingu mzee huyo wa kanisa na kuongoza safari ya kuelekea kanisani.
Wakiwa kanisani hapo polisi
walijitambulisha na kuwauliza wachungaji pamoja na waumini wa kanisa hilo kama
walimfahamu mzee huyo wa kanisa.
Kundi la wazee pamoja na vijana wa kanisa hilo walikiri kuwa Luca ni mmoja wa wazee wa kanisa hilo ndipo polisi hao wakamruhusu kuwakabidhi baadhi ya vitu vyake ikiwemo simu na fedha kisha breki ya kwanza ikawa Kituo cha Polisi cha Tabata-Shule ambapo alifunguliwa jalada la kesi namba RB/3843/2014 -RUSHWA YA NGONO, KUWAWEKA KAMBI KINYUME CHA SHERIA WASICHANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 NA KUWADHALILISHA KIJINSIA.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment