Makaa ya mawe
yakioneshwa kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma
katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
|
Wakala wa
ukaguzi wa madini nchini (TMAA) umeanikiwa kuokoa kiasi kikubwa cha madini yaliyokuwa
yakitoroshwa kinyemela katika viwanja vya ndege nchini.
Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu amesema
kuwa (TMAA) imeokoa zaidi ya bilioni 15
zilizolipwa kama mrahaba tangu ilipoanzisha ukaguzi maalum kwa wasafiri waendao
nje ya nchi.
Bw Mkwizu
amesema hayo alipokuwa akikagua utendaji kazi wa Wakala katika maonesho ya
maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kwa
muda mrefu sasa wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakiitia hasara
Serikali kwa kukwepa ulipaji wa kodi wa madini yaendayo nje ya Tanzania kinyume
na utaratibu uliowekwa.
Naibu Katibu
Mkuu Mkwizu amewasihi viongozi na watumishi wa Wakala kuongeza uchapaji kazi na
uzalendo ili kukomesha kabisa tabia ya wafanyabiashara hao wasio waaminifu.
Afisa Habari wa
Wakala hiyo, Mhandisi Yisambi Shiwa, amesema kuwa bilioni madini yenye thamani ya
shilingi 15.3yaliokolewa katika kipindicha mwaka mmoja, baada ya tambulisha
mpangokazi mpya wa ukaguzi wa ziada katika viwanja vya ndege vikubwa vya Dar es
Salaam, Kilimanjaro na Mwanza, na kubaini wafanyabiashara wasio waaminifu.
Wakala wa
Ukaguzi wa Madini Tanzania ni Wakala wa Serikali ulioanzishwa Novemba 2009,
chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 245. Kwa lengo la kuhakikisha serikali inapata mapato stahiki kutoka kwenye
shughuli za uzalishaji na biashara ya madini nchini.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment