‘Wanasema kampuni za mafuta, Oil
Com, Camel Oil na Lake Oil ni za kwangu, sasa unajiuliza huyo mtu ambae anaweza
akatengeneza kampuni tatu zinazofanya shughuli moja kwa nini asianzishe kampuni
moja ikawa kubwa zaidi ?? kwa hiyo kumekua na manenomaneno mengi, hizo ni
changamoto mfano kwenye siasa huku, watu wengi aidha hawajui nimetokea wapi au
wanajitoa akili katika maana kwamba hawataki kujua nimetoka wapi’
‘Kuna kipindi unaweza ukashangaa
Mwandishi wa habari anachukua kalamu anaandika maneno mpaka unashangaa
kayatolea wapi? sitaki kuamini kwamba Mwandishi unaweza kuandika kwamba
Ridhiwani kapata UNEC kwa sababu ya baba yake, ungechukua muda ukamsoma
Ridhiwani vizuri ukauliza watu waliokaa na Ridhiwani, uliza huyu ameshawahi
kuwa kiongozi??’
‘Wako watu ambao kwa kuwa wamemjua
Ridhiwani baada ya Jakaya Kikwete kuingia Ikulu basi nao wanaanzia hapohapo
Ikulu lakini hawajui Ridhiwani kabla ya baba yake hajawa Ikulu alikua
anaishije, mimi nimekua naishi maisha ya kawaida nimekaa boarding school
nimesoma Mkwawa baba yangu akiwa Waziri, nilikua na uwezo wa kwenda kusoma
Ulaya lakini nimesoma chuo kikuu Dar es salaam pale japo nilikua na uwezo wa
kwenda popote pale ninapotaka ila ni kwa sababu tu mzee wangu alitaka kuona
naishi kama watu wengine’
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment