Walimu hao 97 ni wa katika shule ya
msingi Nyankumbu na Mkombozi wanatumia tundu moja la choo ambacho kiko kwenye
nyumba ya mwalimu, huku wanafunzi 3563 wa shule hizo mbili wakitumia matundu 14,
jambo ambalo limekuwa kero.
Akizungumza na waandishi wa habari shuleni
hapo, mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyankumbu Jasmin Ngume, alisema kuwa
awali ilikuwa shule moja baadaye imegawanywa na kuwepo Mkombozi shule ya msingi
ambapo imeendelea kutumia tundu moja kwa walimu wote huku wanafunzi wakigawana
matundu 7 kila shule.
Ameongeza kuwa kwa mjibu wa taratibu
za wizara uwiano wa vyoo walimu wa kiume 4 hutumia tundu moja na walimu
wa kike 3 hutumia tundu moja, na wanafunzi wakiume 3 hutumia tundu moja na
wakike 4 hutumia tundu moja.
Aidha mwalimu huyo amesema kuwa
kumekuwepo na sintofahamu ya namna ya kujisaidia kwa walimu na wanafunzi, kiasi
kwamba wamekuwa wakienda kwenye nyumba za majirani na hata kuzuiliwa na
kuambiwa kuwa wanavyoo jambo ambalo linawasababishia wakati mwingine kurudi
nyumbani ili wakajisaidie huku muda wa kazi ukiwa bado anahitajika shuleni.
Uchunguzi wa mwandishi umebaini kuwa
shule hii ya muda mrefu awali ilikuwa ni ya ufundi na majengo ambayo yalikuwepo
kipindi cha ufundi ni asilimia kubwa ndiyo yanayotumika kipindi kile huku kwa
sasa shule ikipanuka na kuwa na wanafunzi wengi zaidi.
Baadhi ya wanafunzi walioongea na
mwandishi wamedai kuwa usumbufu wanaoupata unawasababishia kutosoma kwa raha na
wakati mwingine wanahofia kula wakati wanakuwa na njaa kwa sababu itawalazimu
waende nyumbani.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment