Wanachama CUF wilayani Geita mkoani Geita
kimerushiana ngumi na baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama na kusababisha
kuairisha uchaguzi baada ya kutuhumiana kuwepo na mamluki katika ukumbi wa
uchaguzi.
Tukio hilo limetokea juzi katika
ukumbi wa classic mjini hapo baada ya pande mbili zinazovutana kati ya katibu
wa sasa Jovin Mtagwaba na wa zamani Severine Malugu kwa wafuasi wao kutaka mtu
wao apite hivyo kutuhumiana kuwepo kwa kata ambazo hazina wajumbe halali huku
waliopo wakizidi idadi yao.
Katibu wa wilaya Jovin Mtagwaba
alipoulizwa kuhusu kutofanyika kwa uchaguzi huo alisema kuwa kilichokuwa
kinafanyika ni uhakiki wa wajumbe kwanza ambao unafanywa na msimamizi wa
uchaguzi,pili ni kusoma taarifa ya chama na tatu kujiuzuru uongozi, kwa hiyo
ulipoanza uhakiki baadhi ya kata za Katoma,Nyachiluluma,Nzera na Nkome hazikuwa
zimeleta taarifa za uchaguzi wa kata zao wilayani ili tuzitambue na badala yake
taarifa walizipeleka taifani.
Naye Seveline Malugu mgombea katibu
alisema kuwa’’ kuna baadhi ya kata kama za Nzera,Bulela,Kasamwa na Kalangalala
hazina wajumbe halali wamepandikizwa tu kwa ajili ya kuharibu uchaguzi kwani
kata hizo hazikufanya uchaguzi na hazina wananchama wa kutosha yaani hakina
wanachama huko, sasa hawa wanacham wametoka wapi?’’
Kwa upande wa msimamizi wa uchaguzi
kutoka makao makuu ya chama taifa Yusuph Mbungilo alisema kuwa uchaguzi
umeairishwa hadi utakapotangazwa tena kutokana na taratibu za kiuchaguzi
kutozingatiwa.
Baadhi ya wanachama wamedai kuwa
kumekuwepo na mvutano baina ya pande mbili zinazovutana juu ya uongozi, kiasi
kwamba kuwepo kwa mamluki ndani ya ukumbi ambapo majina yaliyokuwepo kwenye
orodha walikuwa wakiitwa majina tofauti, mfano mwanaume anaitika mwanamke jambo
lililowafanya kutoamini pande hizi mbili huenda zimeleta mamluki kwenye
uchaguzi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment