Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya
Kusini ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God
Tanzania (EAGT), Joseph Matare amejiuzulu nafasi yake hiyo kutokana na kanisa
lake kuwataka wachungaji wake ambao ni viongozi wa vyama vya siasa kuachana na
nafasi zao za kisiasa.
Joseph Matare akizungumza na
waandishi wa habari mjini Songea amesema kuwa ameamua kujiuzulu nafasi yake ya
uongozi wa Chadema Kanda ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na
Ruvuma baada ya kanisa lake katika mkutano wake wa kanda kuagiza wachungaji
wake ambao ni viongozi wa siasa kuachia nafasi zao na badala yake wasimamie kazi
ya Mungu katika makanisa yao.
“Kufuatia
maagizo ya mkutano huo wa kanisa uliofanyika Njombe nimeamua kutii... nimeamua
kujiuzulu na katibu wangu mkuu, Dk Willibrod Slaa nilimjulisha tangu tarehe 4
Juni mwaka huu,” alisema Matare katika taarifa yake
ya kujiuzulu.
Amefafanua kuwa muda wa viongozi wa
kanda ulikuwa ni wa muda na wa mpito hadi uchaguzi wa kanda utakapopita ambao
ulipaswa kufanyika Juni 2014 na kwamba muda umeongezwa hivyo ameona aheshimu
maagizo yaliyomweka madarakani.
Hata hivyo, Matare anasema kuwa
anawatia moyo makamanda wote wa Chadema waliobaki kuendelea kupigania nchi ili
iondokane na uovu unaotendeka sasa na kwamba Mungu atakuwa nao wale wote
wanaotafuta haki kwa ajili ya wananchi walio wengi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment