Mtu mmoja ambaye hakutambulika jina
lake mara moja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 38 (mwanaume) kufa papo hapo
Na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kugongwa na basi la Lushanga kwenye makutano ya barabara ya
Kamanga na Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Tukio hilo limetokea jana Juni 30
majira ya saa 9 alasiri ambapo basi la abiria mali ya kampuni ya Lushanga lenye
namba za usajili T 312 ATA likiwa na Abiria likitokea Mkoa wa Geita kuleleka
mkoani Mwanza kupitia kivuko cha Kamanga.
Marehemu alikuwa anaendesha troli
lililokuwa limebeba miti ambapo amepasuka kichwa na kusababisha Ubongo kutoka
nje, na mwili wake umepelekwa katika hospitali teule ya wilaya ya Sengerema kwa
ajili ya uchunguzi zaidi pamoja na majeruhi kwa ajili ya matibabu.
Kwa upande
wa mashuhuda abiria waliokuwa katika basi hilo hakuna aliyejeruhiwa katika
ajali hiyo pamoja na gari hilo kuharibika baada ya kushindwa kuendelea na
safari hivyo kurudi nyuma na kujikita kwenye mtaro.
Hadi
tunaandika habari hii chanzo cha ajali hii hakijajulikana kutokana na uchunguzi
wa polisi wilayani humo kuhusu ajali hiyo kuendelea na dereva wa basi hilo na
konda wake waliotokomea kusikojulikana kutokana na mkusanyiko wa watu eneo la
tukio.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment