Shirika
la jambo Bukoba mkoani kagera linalofadhili ujenzi wa maktaba
katika shule ya msingi Bihororo wilayani Ngara limeiomba ofisi ya
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo kuchangia baadhi ya vifaa katika
maktaba hiyo.
Mratibu
wa shirika hilo Bw Steven Gonzaga amesema hayo wakati wa ukaguzi wa jengo
la maktaba hiyo iliyofadhiliwa kwa thamani ya Shilingi milioni nne ambapo jamii
inachangia ujenzi huo kwa asilimia 25 ya fedha iliyopangwa.
Bw
Gonzaga amesema kuwa wananchi wa Buhororo wamekusanya mawe mchanga matofali na
kokoto pamoja na maji hivyo na kwa kuwa fedha haitoshelezi
halmashauri haina budi kusaidia ili maktaba ikamilike kwa wakati.
Hata hivyo mwakilishi wa Afisa elimu
idara ya msingi wilayani Ngara Bi Grensia Rwela ameshauri katika ujenzi
huo pawekewe miundombinu rafiki ya watoto wenye mahitaji maalumu ili nao waweze
kupata haki yao ya kuitumia maktaba.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment