Ziara ya
wahandisi hao wa TANESCO inalenga katika kuwawezesha katika kukabiliana na
matumizi ya nguzo zisizo na ubora na ili kuongeza ufanisi na usalama katika
zoezi la kusambaza umeme nchini.
Wahandisi hao
wamepata fursa ya kutembela kiwanda cha Sao Hill kilichopo Mafinga mjini Iringa
ikiwa ni mafunzo kwa vitendo juu ya utambuzi wa nguzo bora.
Washiriki
waliweza kuona namna uzalishaji na utayarishaji wa nguzo unavyofanyka ikiwa ni
pamoja na ukaguzi wa nguzo kabla haijawekewa dawa na ukaguzi wa nguzo baada ya
kuwa ya kuwekewa dawa.
Akivitaja vitu
vinavyoangaliwa kabla nguzo haijawekewa dawa Bw. Emmanuel Simkoko ambae ni
mkaguzi kutoka Kampuni ya Ukaguzi wa Ubora ya SGS ya jijini Dar es Salaam,
alisema vitu vya kuzingatia katika zoezi la utambuzi wa ubora wa nguzo ni
pamoja na aina ya mti unaotumika katika kuandaa nguzo hizo, ukubwa, pamoja na
kimo cha nguzo husika.
“Kuna vitu vya
kuzingatia wakati wa kuchambua aina ya ubora wa nguzo, ni muhimu kujua aina ya
mti ili kubaini hali ya unyevunyevu, na masuala mengine ya utaalamu
ikiwamo vipimo vya nguzo husika,” alisema Bw. Simkoko.
Kwa mujibu wa Bw.
Simkoko, nguzo bora haitakiwi kuwa na hali ya unyevunyevu kuvuka 25%, pamoja na
ukubwa wa kitako cha nguzo kisipungue milimita 20 na juu ya nguzo isipungue
milimita 20.
Wahandisi hao
walielimishwa sifa nyingine ya nguzo bora kuwa ni pamoja na kuangalia nguzo
kama imeliwa na wadudu, umbo la nguzo iliyo panda haifai kwa kuwa haitoweza
kukidhi kazi husika.
Bw. Simkoko
alihitimisha kwa kuwaelimisha wahandisi hao namna ya kuwekea dawa nguzo zilizo
bora, “Baada ya nguzo kuwekewa dawa huwafanyiwa majaribio kuangalia dawa kama
imewekwa ipasavyo, na tuna utaratibu wa kuzifanyia majaribio kila mwezi,”
aliongeza Bw. Simkoko.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment