Kikundi
cha Wanawake Wajasiriamali, kinachojihusisha na Usindikaji wa vyakula manispaa
ya Bukoba kimepatiwa wa Baiskeli 39 ili ziweze kuwasaidia Wajasiriamali hao
katika shughuli zao za uzalishaji.
Picha juu ni Bi Ziporah Pangani, mkuu wa wilaya Bukoba, akipewa maelezo na mratibu wa kikundi Bi Jesca Jonathan, alipowasili kwenye ofisi yao.
Akikabidhi
Baiskeli hizo, mkuu wa wilaya ya Bukoba , ZIPORAH PANGANI amewahimiza wanawake
hao kuendelea na umoja huo, kwani
kupitia kikundi hicho wameweza kufanya shughuli zao za kimaendeleo.
Akisoma
risala ya wana kikundi, Mratibu wa
kikundi hicho JESKA JONATHAN amesema kuwa, kikundi kina jumla ya wanachama 425
ambao wamekuwa wakijihusisha na shughuli za kilimo na usindikaji vyakula.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment