MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 4 August 2014

MAMA AJIFUNGUA WATOTO WANNE KWA WAKATI MMOJA GEITA


Mama mmoja Tecra Kazimili(24) mkazi wa Lubili katika wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, amjefungua watoto (4) kwa wakati mmoja huku mtoto mmoja wa kiume amefariki muda mfupi baada ya mama huyo kujifungua.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kushuhudia tukio hilo ambalo si la kawaida,  mama Tecra alisema hii ni mara yake ya nne kujifungua lakini ni mara yake ya kwanza kujifungua watoto wanne kwa wakati mmoja.

Tecra ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi katika Hospitali ya wilaya ya misungwi Mkoani Mwanza,  alisema anamshukuru Mungu kwa kumjalia Afya njema na kumuwezesha kujifungua watoto (4) pamoja na kwamba mmoja wa watoto hao amepoteza maisha muda mfupi baada ya kuzaliwa. “yote ni mipango ya mungu.”alisema Tecra

Tecra  aliongeza kuwa uzao wake ya nne lakini hana mtoto hata mmoja kutokana na watoto wake wote (3) kufariki wanapofikisha mwaka mmoja hadi mmoja na nusu kitendo kilichosababisha kufukuzwa na mume wake Mussa Masalu aliyekuwa anaishi naye baada ya kuona watoto wanafariki na kudaiwa kuwauwa yeye mwenyewe jambo ambalo halina ukweli,alisema Tecra.

Pamoja na hayo Tecra  anawaomba Watanzania wasamalia wema watakaoguswa wamsaidie kwa kuwa huyu aliyempa mimba hiyo si mumewe hivyo hana msaada wowote atakaopata wakati atakapokuwa anaendelea kuwalea watoto wake hao.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Marco Mwita aliwaambia waandishi wa Habari kuwa tukio hili ni si la kawaida kutokea mara nyingi wakina mama wamekuwa wakijifungua watoto watatu na si wanne kama ilivyotokea kwa Tecra.

Na Mwanaharakati.

No comments: