MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 9 August 2014

NEWS ALERT!!! FAINI KWA WAKULIMA KUSHINDWA KUNG'OA MIGOMBA ILIYOAMBUKIZWA UNYANJANO KAGERA, YALALAMIKIWA NA WAKULIMA KATIKA MAONESHO YA NANENANE.

 Wameongeza kuwa, wanapotoa malalamiko yao kwa uongozi, wanaambiwa kuwa hakuna maofisa ugani wa kutosha kumfikia kila mkulima, uhaba wa vyombo vya usafiri pamoja na ubovu wa miundombinu.

Katika kujikwamua wenyewe, wakulima wameeleza kuwa wamekuwa wakulima na wafanyabiashara kwa wakati mmoja, kwani baada ya kulima wengine wanasindika mazao yao kwa kutengeneza vyakula kama CHICHILI, UNGA, MIKATE, KEKI na vinywaji kama JUICE, na WINE, ambavyo vyote vinatokana na Ndizi, Mhogo, Karanga, Viazi na matunda.
Mwandishi Mac Ngaiza, katika banda la MAYAWA akipata maelekezo ya matumizi ya unga wa ndizi na Vanila.

Mwenyekiti wa kampuni ya Ndizis Bi. ADELINA akizungumza na mwanahabari jinsi wanavyosaidia wananchi kusindika mazao yao ili yasiozee shambani kwa wanaweza kusindika.

Picha juu na chini, ni wakulima wa Halmashauri mpya ya wilaya Kyerwa, wakieleza kuwa wao ni wakulima na maeneo yao ya rutuba ya kutosha na wanajitahidi kulima, lakini wanakumbana na changamoto ya watalaamu.

Picha juu ni Wataalamu wa VETA wakitoa maelezo kuhusu ukarabati wa magari, na chini mtaalamu wa MAGEREZA akifafanua faida za kulima bustani, huku akiwataka wakulima kukubali kubadilika katika mawazo ya kulima mazao mbadala wa ndizi na muhogo ambao unashambuliwa na magonjwa.


Juu ni ndizi aina ya Nshakala na chini Mhogo aina ya Lushura inayolimwa wilayani Kyerwa.

Baadhi ya vyakula vilivyosindikwa Chichili na Keki.
 Na Mwanaharakati.

No comments: