MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 1 August 2014

NEWS ALERT!!! RAIS KIKWETE ASISITIZA KUWA ALIKUWA SAHIHI KUTOA MAONI YA KATIBA ALIPOHUTUBIA BUNGE LA KATIBA.



Silioni kosa langu kwa kufanya hivyo, kwani Rasimu imetolewa hadharani kwa watu kuijadili.  Na mimi kama raia ninayo haki ya kufanya hivyo kama wafanyavyo wengine.  Kwa nini nilaumiwe kwa kutumia haki yangu hiyo.  

Lakini, pia mimi ndiye Rais wa nchi yetu, ninayo dhamana ya uongozi na ulezi wa taifa letu.  Itakuwaje kwa jambo kubwa la hatma ya nchi yetu nilinyamazie kimya.  Watanzania wangeshangaa na wangekuwa na haki ya kuhoji Rais wao ana maoni gani.  Bahati nzuri nilitoa maoni yangu mahali penyewe hasa, na kwa uwazi, kwenye Bunge Maalumu la Katiba.  Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kuwa namna nilvyotoa maoni yangu sikuwa natoa maagizo wala kushurutisha, ndiyo maana kila wakati niliwakumbusha Wajumbe kuwa mamlaka ya uamuzi ni yao. Yangu yalikuwa maoni tu wanahiyari ya kuyakubali au kuyakataa.   Niliwataka Wajumbe wasome na kuielewa vyema Rasimu.  Nilisema wasome sura kwa sura, mstari kwa mstari na neno kwa neno.  Niliwaomba wajiridhishe kuhusu uandishi na dhana mbalimbali.  Nilitoa mifano ya mambo yahusuyo uandishi ambayo ni vyema wayatazame.  Pia nilitoa mifano ya dhana ambazo niliwasihi wajiridhishe juu ya kufaa kwake kuwepo.

  Kuhusu muundo wa Serikali tatu, nilieleza wazi kuwa sina tatizo nao kama ndiyo matakwa ya Watanzania.  Lakini, nilieleza hofu yangu kuhusu mapendekezo ya Tume na kuwataka Wajumbe wafanye kazi ya ziada kuondosha udhaifu iwapo wataukubali muundo unaopendekezwa.  Nilieleza nia yangu ya kutaka tuwe na Serikali ya Muungano yenye ukuu unaoonekana, yenye nguvu ya kuweza kusimama yenyewe, inayoweza kuwa tegemeo kwa nchi Washirika, Serikali isiyokuwa tegemezi wala egemezi kwa nchi washirika na ambayo inavyo vyanzo vya uhakika vya mapato.  Hivi kwa kutoa ushauri huo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba inageuka kuwa nongwa.  Kwa kweli sielewi lawama ni ya nini?. 

Naamini sistahili lawama bali pongezi kwa kuwa muwazi na kutoa ushauri wa msingi ambao utasaidia nchi kupata Katiba nzuri inayojali maslahi ya watu wa nchi yetu na ya nchi zetu mbili zilizoungana miaka 50 iliyopita.  
 

Na Mwanaharakati.

No comments: