Wakaazi
wa Kata Katoma Bukoba vijijini, wamelalamikia utaratibu wa halmashauri kuziba
barabara inayotumiwa na kata mbalimbali za wilaya ya Bukoba na Misenyi.
Wakizungumza
na mtandao huu kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema kuwa wanashangaa kuona
kumerundwa vifusi katika barabara ya Katoma- Ishozi kwa muda mrefu, huku
serikali ikishindwa vikisambaza jambo ambalo pamoja na kuwazuia kusafirisha
bidhaa zao kwa uraisi, pia imekuwa shida kwa kusababisha ajali za mara kwa
mara.
Wamesema
hali hiyo imetokana na kutumika upande mmoja mdogo wa barabara uliosalia, kwani
vifusi hivyo vya molam, vimerundwa katikati na kuachana nafasi ndogo ya
watembea kwa mguu ambapo wanasema kuwa vifusi hivyo vimekaa kwa zaidi ya miezi
miwili sasa.
Barabara
hiyo hutumiwa na wakaazi wa Bukoba vijijini na wa wilaya ya Misenyi, kwa kata
za Ishozi, Kanyigo na wanaoelekea mpakani mwa uganda upande wa Kiziba kwa
kusafirishia bidhaa zao na mazao ya kilimo kama kahawa, ndizi na muhogo.
Jitihada
za kutafuta uongozi wa halmashauri kuzungumzia hilo zinaendelea, ilhali
tukimtafuta mkandarasi wa eneo hilo linalokadiriwa kuwa na urefu wa kilomita
zaidi ya 10.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment