
Mashuhuda wa ajali hiyo walidai kuwa
chanzo chake ni gari hilo ambalo walikuwa wakisafiria kutoka Lupingu - Ludewa
kufeli breki na hivyo kupinduka .
Inadaiwa baada ya gari hilo aina ya
Toyota Coaster inayojulikana kwa jina la DMX kufeli breki dereva aliwataka
abiria kutulia ndani ya gari hilo ila diwani huyo hakuweza kufanya hivyo na
kuamua kuchukua maamuzi magumu ya kutaka kuruka katika gari hilo ambapo wakati
akiruka alimsukuma utingo wa basi hilo na hivyo wote wawili utingo na diwani
kufunikwa na gari hilo na kupelekea kifo cha diwani huku utingo akiwa mahututi
baada ya kubanwa na gari hilo.
"Diwani amepoteza maisha wakati
akiwa njiani kuelekea kujumuika na wananchi wake katika shughuli ya maendeleo
ya kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kuelekea kijijini kwake Lupingu"
Alisema mmoja wa abiria.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo
Filikunjombe ameeleza kusikitishwa na kifo cha diwani huyo kutokana na mchango
wake mkubwa aliouonyesha enzi wa uhai wakati kwa kushiriki vema na wananchi wa
kata yake katika zoezi la kufyeka na kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kwenda
Lupingu.
Alisema kuwa anakumbuka ni wiki
mbili pekee zimepita toka diwani huyo alipoungana nae katika uchimbaji wa
mashimo ya nguzo za umeme kwenda kijiji cha Ntumbati na kuwa hata wakati ajali
hiyo inamkuta bado alikuwa katika harakati za kuwatumikia wananchi wake.
"Ludewa tumempoteza diwani
mchapa kazi na aliyependa kujituma muda wote na hata wakati mwingine diwani
huyo alikuwa akifanya kazi ngumu kama mwanaume kwa kubeba nguzo za umeme kwa
kushirikiana na mimi na wananchi wake.....kwa kweli kifo chake ni pigo kubwa
ndani ya CCM na kwa wananchi wa kata nzima ya Lupingu"
Kwani kati ya madiwani waliokuwa
bega kwa bega na wananchi wao na mbunge ni pamoja na diwani huyo ambaye alikuwa
mstari wa mbele kuona Kata ya Lupingu inapata umeme wa uhakika baada ya miaka
zaidi ya 50 ya Uhuru bila umeme .
Mbunge Filikunjombe alisema
atamkumbuka diwani huyo kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo na
vile alivyofanya kazi na wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa, Juma Madaha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha kifo cha diwani huyo na kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2 asubuhi .
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment