MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday 4 September 2014

MEYA WA ILALA AZUNGUMZIA TUHUMA ZA MACHINGA COMPLEX DHIDI YAKE.





Halmasahuri ya Manispaa ya Ilala imesikitishwa sana na habari za upotoshwaji zilizofanywa na wanaojiita viongozi wa soko la Machinga complex zikimlenga Mstahiki Meya wa Halmashauri Mhe.Jerry Silaa.

Ieleweke wazi soko la Machinga Complex linamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na lina Bodi na Manejimenti ya Soko, kikundi cha watu wanaojita viongozi hawako kisheria lakini ndio walewale waliochangisha fedha kwa wafanyabiashara kinyume cha sheria na kujenga mabanda kuzunguka soko zima ambayo Halmashauri iliyavunja.

Jitihada Mbalimbali zimefanywa na Halmashauri hizi mbili kuhakikisha soko hili linapata ufanisi. Mhe Said Meck Sadiki Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alisimamia jitihada hizi ikiwemo ujenzi wa kituo cha basi mtaa wa New Kisutu.

Halmashauri inamshukuru Katibu Mkuu wa Tamisemi Jumanne Sagini katika ziara yake alitoa 250m kwa ajili ya ujenzi wa kituo. Halmashauri ilitangaza zabuni tarehe 27/5/2014 na ilifunguliwa 27/6/2014 taratibu za kisheria za uchambuaji ziliendelea na mwezi July bodi ya zabuni ilikaa na ilishindwa kupitisha zabuni hiyo kwani mkandarasi aliyependekezwa aliomba kazi hii kwa 332m ambazo ni sawa na 82,550,500 zaidi ya fedha zilizotengwa ambazo ni 250m. 

Jitihada za kupata fedha za nyongeza zimefanyika na tayari Mstaiki Meya Jerry Silaa ameridhia kuongeza fedha hizo toka kwenye mradi mwengine wa halmashauri.

Maombi haya yatapata ridhaa ya kamati ya fedha na utawala chini ya mwenyekiti wake Mhe.Jerry Silaa kitachokaa tarehe 3/9/2014Tunategemea kazi ya ujenzi kuanza wakati wowote baada ya fedha kuidhinishwa.

Halmashauri inaendelea kuutaka umma kutafuta taarifa toka vyanzo sahihi na kuepuka kupotosha umma. Vilevile kujihusisha na taratibu za utendaji kazi wa serikali. Mstaiki meya ni kiongozi wa juu wa halmashauri na hana mahusiano ya moja kwa moja ya matumizi ya fedha za serikali zaidi ya majukumu ya usimamizi.

Inaonyesha wazi watoa habari walikuwa jambo lingine la kisiasa lililojificha nyuma ya pazia aidha kutumika, ujinga au kutafuta “kiki” kupitia jina la Meya. Binafsi mstaiki amepuuzia na anavishauri vyombo vya habari kujielekeza kwenye weledi wakati wa kutoa habari kwa kuzingatia uhalali wa chanzo,mashiko ya kisheria ya habari yenyewe kuepuka kujiondolea imani kwa umma kwa tamaa ya umaarufu wa haraka.

Imetolewa na Ofisi ya Mstaiki Meya
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
 Na Mwanaharakati.

No comments: