Mchungaji James |
Hatahivyo mashirika,
Taasisi na watu binafisi mkoani Kagera wameombwa kuendelea kuchangia katika miradi
mbalimbali ya Maendeleo .
Wito
huo umetolewa na mmoja wa wadau wa maendeleo manispaa ya Bukoba, MCHUNGAJI KING
JAMES wa kanisa la ukombozi manispaa ya Bukoba wakati wa hafla ya kukabidhi
mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara unaondelea kwa
sasa.
Mchungaji
JEMES amesema kuwa amewiwa kutoa mchango
huo, katika shule za manispaa zinazoendelea na ujenzi huo ili kuunga mkono
juhudi za serikali katika kuboresha elimu hususan masomo ya sayansi.
Kulia ni mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi ZIPORAH PANGAN |
Kutoka kushoto ni mkurugenzi manispaa, naibu meya Ngalinda, mchungaji James, mwenyekiti wa ccm wilaya, na afisa tarafa Abdon Khawa. |
Ameongeza
kuwa juhudi za serikali pekee hazitoshi katika kuwaletea wananchi maendeleo
bali ni kushirikiana na wadau wote.
Akisoma
risala wakati wa kupokea msaada huo mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba, ADOH
MAPUNDA amesema kuwa msaada huo, umetolewa kwa wakati muafaka na kutaka msaada
huo kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment