MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 10 September 2014

NEWS ALERT!!!WANANCHI WAMLILIA RPC LEONARD PAUL KURUDI GEITA



Baadhi ya wananchi wilayani Geita Mkoani Geita wamemuomba (IGP) Ernest Mangu kumrudisha aliyekuwa kamanda wa Mkoani Geita Leonad Paulo aliyeamishiwa Mkoa wa Marogoro hivi karibuni.
IGP ERNEST MANGU
Wakiongea kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamefikia uamuzi huo kutokana na kukithiri kwa mauaji yanayosababishwa na majambazi ambao wamefanya wakazi wa mji huu kukosa amani na kushindwa kufanya kazi zao za kila siku kwa kuogopa kuvamiwa.
RPC Morgroro Leonard Pul

RPC Geita Joseph Konyo

Mmoja wa Mwananchi aliyejitambulisha kwa Jina la Mashanja Juma kutoka Katoro wilayani humo, alisema kuwa wakati wa kamanda Paulo majambazi waliisha na mauaji ya vikongwe yalipungua kwa kasi, lakini kwa sasa vikongwe wanazidi kukatwa na kuuawawa huku majambazi wakizidi kumaliza maisha ya ndugu na jamaa zao.

Juma aliongeza kuwa Matukio makubwa ambayo yametokea kwa kipindi cha  muda mfupi tangu kamanda Paulo aondoke ni pamoja  kuwavamia wafanyabishara wawili na kumua mmoja wao Gozibati Walwa, ambapo walichukuwa pesa na bastola.

Alilitaja tukio la pili kuwa ni kuteka kituo cha polisi Bukombe na kuua askari wawili ambao ni PC Dastan Kimati(25) na Horia Mwandija(30)  na kujerui wawili, Mohamed Hassan(25 na Devis Ngutama(44) pia walibeba bunduki na mabomu pamoja na risasi na kutokomea, japo bunduki inasemekana zimekamatwa lakini wananchi bado wana hofu kubwa.

Wananchi wa Geita wanasema wakati wa uongozi wa RPC Paul mkoani humo, ofisi yake ilikuwa wazi kila wakati  kwa watu wote ndio maana alipelekewa tarifa za tatizo na kulifuatilia mara moja, alisema Juma.

Matukio ya kuendelea kuuawa kwa watu yamezidi kuwafanya wakazi wa mji huo kutofanya kazi zao kwa uhuru, hivyo kumuomba IGP kutenga kanda maalumu katika mkoa wa Geita, Huenda ikapunguza mauaji.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: