Na Valence Robert Geita.
WANANCHI Mkoani Geita wametakiwa
kuacha mara moja tabia ya kuwaua vikongwe kwa imani za kishirikina
na kuacha kujichukulia sheria mikononi kwani kufanya hivyo wanakwenda kinyume
na mapenzi ya Mungu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Asikofu
wa kanisa la Habari Njema, Tryphone Siku, wakati wa kufungua mkutano wa siku
tano katika viwanja vya shule ya msingi kalangala vilivyoko mjini hapa. Lengo
likiwa ni kuwaombea watu kuacha dhambi na kumrudia mwenyezi Mungu.
Tryphone alisema kuwa watu wa Mkoa
huo wamekuwa wakiwaua vikongwe kwa imani za kishirikina na kujichukulia sheria
mikononi kwa kuwauwa wahalifu hivyo kuwaomba kuacha mara moja kwani wanakwenda
kinyume na mapenzi ya Mungu na kuwataka, waganga wanaopiga ramli chonganishi
nao kuacha.
Aliendelea kusema kuwa
viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa
huo Said Magalula wamekuwa wakijitahidi sana kuwaelimisha wananchi kuacha tabia
hizo kwa kushirikiana na makanisa likiwemo kanisa lake.
Naye Mchungaji wa kanisa hilo Alex
Mshindi kutoka Rwanda alishukuru wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano
huo lakini akawaomba wakazi wa Mkoa wa Geita kwa ujumla kuwa wanatakiwa
kumrudia aliyewaumba na kuacha matendo maovu.
Nimeshangazwa na mauaji ya vikongwe
na kujiochukulia sheria mikononi ninavyosikia hapa Mkoani kwenu
jamani acheni tabia hizo lakini tushirikiane kuwaombea wanaofanya hivi waache
na wamrudie muumba wao. Alisema Alex.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment