Baba Levo anasema alizitoa hizo taarifa saa tisa
mchana sababu ndio aliweza kupata angalau network ya mtandao wa simu kwani kwa
saa mbili zilizopita alishindwa kupiga simu baada ya kupata ajali porini
kutokana na uzembe wa dereva wa Coaster aliehama upande wake na kuhamia upande
wa pili kukwepa barabara mbovu.
Kina Baba Levo walikua kwenye Basi kubwa
lililogongana uso kwa uso na Coaster ambapo Baba Levo alikua amekaa pale mbele
pembeni kabisa ya dereva kwenye kile kigodoro ambapo msanii huyu ilibidi akae
hapo sababu ticket yake iliuzwa kwa watu wawili hivyo aliamua kuiachia siti
yake kwa mama wa Kiarabu baada ya kujikuta wote wamepangwa siti moja.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment