BAADA ya kuvuja kwa
picha katika mitandao ya kijamii zaidi ya wiki moja iliyopita, zikionesha
askari wawili wa usalama barabarani wakiwa ‘kimahaba’ ndani ya sare za kazi na
kusababisha kupoteza ajira zao kutokana na kukiuka maadili, siri zaidi nzito
zimezidi kuvuja kuhusiana na ishu hiyo na Amani limemuibua afande wa kike baada
ya kumsaka sana.

Askari aliyefukuzwa kazi kutokana na
kosa la ukiukaji wa maadili, Veronica Mdeme.
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka wilayani
Misenyi mkoani Kagera, askari wa kike aliyeonekana kwenye picha hiyo chafu, WP.
8898 Veronica Mdeme, inadaiwa kuwa alipata uhamisho kutoka polisi mkoani humo
na kupelekwa katika wilaya mpya ya Misenyi mwaka 2011 ambako mwaka mmoja
baadaye, ndipo akapigwa picha hiyo iliyoleta gumzo kubwa ndani na nje ya Bongo.
Ilidaiwa kwamba, picha hiyo ilipigwa
katika barabara ya lami iendayo Mutukura, umbali wa Kilomita 50 kutoka Misenyi
na kwamba askari hao walikuwa katika Kituo cha Polisi cha Kyaka.
Nguzo ya umeme inayoonekana nyuma yao, ni zile zinazopeleka umeme nchini Uganda kutoka Bwawa la Umeme la Mtera, Tanzania.
ILIKUWA PICHA YA KISHKAJI TU LAKINI…
Habari zilidai kuwa, askari hao Veronica, F.7788 Mpaji Mwasumbi na PC Fadhil Linga, walikuwa zamu moja na kwamba picha hiyo ilipigwa katika mazingira ya kishkaji tu lakini baadaye ikaja kuzua balaa kubwa.

Ilisemekana kwamba, Linga ndiye
aliyewapiga picha wenzake ambao habari zisizothibitishwa zilisema kuwa walikuwa
na uhusiano wa kijamii.
Madai yalizidi kutiririshwa kwamba
baada ya kupigwa kwa picha hiyo, Linga alibaki na nakala katika kamera yake kwa
muda wa miezi kadhaa kabla ya kugundua kuwa kumbe ilikuwa ni dili.
AWAGEUZIA KIBAO
Ilidaiwa kwamba, katika hali isiyotarajiwa, Mpaji na Veronica hawakuamini masikio yao baada ya Linga kuwaambia kwamba alihitaji kupata ‘kitu kidogo’ kutoka kwao ili aweze kuendelea kuhifadhi siri ya picha hizo.

Ilisemekana kuwa afande huyo
aliwaambia wawili hao kama ataivujisha picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii,
watapoteza kazi.
“Baada ya kuambiwa hivyo, jamaa
walilegea kabisa. Mwanzoni walitia ngumu lakini walipoona jamaa amekomaa,
hawakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana naye, hivyo akawa anapata kitu kidogo
kila alipojisikia na kuwa nipe nikupe na hakuna uhakika kama dada Vero
alisalimika kwenye mambo mengine kwani naye alikuwa akitumia nguvu kubwa
kuhakikisha mumewe hajui,” kilidai chanzo hicho.
![]() |
Veronica Mdeme akiwa kwenye pozi.
|
WAAMUA KUJILIPUA, WAMSHTAKI
Ilielezwa kwamba, baada ya ‘kutolewa upepo’ kwa muda mrefu na kuonekana kama wangekuwa ATM ya kudumu ya Linga, Mpaji na Veronica waliamua kujilipua na kwenda kumshtaki kwa kigogo wa juu wa jeshi la polisi mkoani humo ambaye anatajwa kuujua mchezo mzima ulivyokuwa.

Ilisemekana kwamba, kiongozi huyo
alilichukulia jambo hilo kwa uzito wake na kuwakalisha wote watatu ili
kuzungumza nao.Iliendelea kudaiwa kuwa katika kikao kati ya askari hao na bosi
wao, wawili hao walikiri kupigwa picha hiyo na kuomba msamaha, lakini wakamlalamikia
mwenzao ambaye naye alikiri kufanya kitendo hicho, kwa kuwageuza kuwa ATM.
Ilidaiwa kuwa mkubwa huyo alimuamuru
Linga kuzifuta picha hizo na kuwataka kusameheana, kwani kitendo walichokifanya
ni kibaya na kinachoweza kuhatarisha ajira zao. Linga alikubali ‘kuzi-diliti’
picha hizo!
WAGAWANYWA, LINGA ARUDIA
Ikazidi kudaiwa kuwa ili kuwafanya waishi kwa amani, waligawanywa katika vituo tofauti vya kazi mkoani humo huku mmoja wao, Mpaji akipelekwa Dar ambako alikwenda kusoma Chuo cha Polisi Kurasini.
Ikazidi kudaiwa kuwa ili kuwafanya waishi kwa amani, waligawanywa katika vituo tofauti vya kazi mkoani humo huku mmoja wao, Mpaji akipelekwa Dar ambako alikwenda kusoma Chuo cha Polisi Kurasini.
“Wakiwa katika vituo hivyo tofauti,
Linga alitulia kwa muda mchache tu kabla ya kuanza tena usumbufu wake, hasa kwa
Veronica ambaye anadaiwa kuwa mke wa mtu. Ni katika usumbufu huo wa mara ya
pili, akina Mpaji wakaamua kumjibu jeuri jamaa, hawakuwa na uoga tena kwa vile
suala lao lilishafahamika kwa wakubwa,” kilisema chanzo chetu.
Inaelezwa kwamba majibu ya jeuri
kutoka kwa Vero na Mpaji yalimuudhi Linga ambaye kwa lengo la kuwakomoa,
aliamua kuzitupa picha hizo katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambako nako
zilizagaa kwa kasi ya moto wa kifuu na kuwafikia watu mbalimbali, ikiwa ni
pamoja na vyombo vya habari vilivyoamua kuripoti.
“Picha hiyo ilipoonekana mtandaoni,
moja kwa moja polisi walijua imewekwa na Linga kwa sababu hakukuwa na mtu
mwingine aliyefahamu kuhusu picha hiyo. Ndiyo maana wote watatu walifukuzwa
kazi siku moja, hawakuwa na sababu ya kuhangaika kujua nani kaweka,” kilisema
chanzo hicho.
PICHA YA MREMBO YAWA GUMZO
Baada ya kufukuzwa kazi kwa wahusika hao watatu, kumekuwa na picha za mrembo mkali ambaye amekuwa akifananishwa na Veronica huku kukiwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kama kweli ni yeye (angalia picha).

Kwa mujibu wa maoni lukuki katika
mitandaoni, kama kweli mrembo huyo ndiye huyo askari wa kike, basi jamaa
aliyekuwa naye kimahaba, alistahili adhabu yoyote kuliko kukosa mahaba hayo.
“Ni kama walivyoimba wale watoto wa
Yamoto Band, yaani nzi kufia kwenye kidonda siyo ufala bali kupenda. Huyu mtoto
mashalaah,” ilisomeka sehemu ya maoni ya stori hiyo ambayo ndiyo habari ya
mjini kwa sasa.
Juzi, Amani lilimtafuta Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe ili kumsikia nini kinaendelea baada ya
askari hao kufukuzwa kazi lakini hakuwa hewani.
Naye msemaji wa Jeshi la Polisi
Tanzania, Advera Senzo alipopigiwa simu na kuulizwa alisema walishafukuzwa kazi
hakuna kingine lakini akaelekeza apigiwe simu Mwaibambe.
Na:Amani GPL
No comments:
Post a Comment