MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 16 October 2014

UFYATUAJI WA MABOMU KAGERA POLISI YATOA TAARIFA

RCO wa polisi mkoani Kagera Gilles Mrotto, ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari kuwa tarehe 14 Oct 2014, saa 11:45 katika barabara ya Kashozi manispaa ya Bukoba askari wa usalama barabarani wanaofahamika kama TIGO ua RIDDER, walikutana na kijana anayeitwa Godfrey Joseph mhaya, akiwa bila helmet yaani kofia ngumu,ndipo wakamsimamisha akakataa kusimama ndipo walipomfuatilia na kufanikiwa kumkamata.
Kijana anayetuhumiwa kuzua vurugu mwenye tishirt nyekundu kushoto akiwa chini ya ulinzi ndani ya gari la polisi.
Wakati wa kumkamata alikuwa akigoma na ndipo zilitokea vurugu baada ya bodaboda wengine waliokuwa wakipita walianza kurusha mawe kuwabonda askari, huku kijana huyo Godfrey anasadikiwa kuwa na mafunzo ya mgambo, alitaka kuwanyang'anya polisi bunduki wakati huo akigundulika kuwa mlevi,  ndipo askari waliamua kutumia nguvu na kufanikiwa kumfikisha kituoni.

Katika purukushani hizo, kioo cha bank ya CRDB ambapo yalifanyika mapigano hayo kilivunjwa ambapo mpaka sasa vijana 12 wapo mikononi mwa polisi baadhi ni waendesha bodaboda kwa uchunguzi na ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Na Mwanaharakati.

No comments: