Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana katika kijiji cha Chekereni
katika mji wa Hedaru Wilayani humo huku pia abiria wapatao wanne waliokuwepo
katika basi hilo wakipata majeraha katika maeneo mbalimbali ya miili yao.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali
hiyo, gari hiyo ndogo yenye namba T 653 BZR iliyokuwa ikielekea mkoani
Kilimanjaro ilitoka na kuingia upande wa kulia na ndipo ilipogongana na basi
hilo lenye namba T 702 BUW lilikuwa likitokea mkoani Arusha.
Jeshi la Polisi Kitengo cha usalama
Barabarani limefika eneo la tukio na kufanikiwa kutenganisha magari hayo,
wakichukua kuku wakichukua viungo vya miili ya marehemu hao ambao hawatambuliki
kutokana na kusagika vibaya.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment