Mamlaka
ya veta kanda ya ziwa imesema zaidi ya sh. bilion 6.7 zitatumika katika ujenzi
wa chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma katika Mkoa wa
Geita.
Kauli
hiyo ilitolewa hivi kalibuni na Charles Kengele mchambuzi wa masoko wa Veta kanda ya ziwa , ambapo alisema mkoa wa Geita umetenga eneo la mita za
mraba 272,700 eneo la Magogo takribani km 12 kutoka Geita mjini.
''Eneo
hili limeshapimwa na mchakato wa kupata hati miliki unaendelea, mamlaka
inatoa shukrani za dhati kwa uongozi wa Mkoa wa Geita ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa
Magalula Said kwa ushirikiano inayotupa''.alisema Kengele.
Katika
hatua nyingine Kengele alisema kuwa serikali yaTanzania na Benki ya Maendeleo
ya Afrika (ADB) zimekwisha tia sahihiya makubaliano ya kugharamia mradi wa
ujenzi wa chuo hicho, ambapo ADB itatoa zaidi ya sh. bilioni 5.7 huku
serikali ya Tanzania itatoa sh. 9.4 milioni na kufanya mradi huo kuwa na
thamani ya Shs. 6.7 bilioni.
Katika
jukumu lake la kutoa elimu na mafunzo ya ufundi stadi, mamlaka inamiliki na
kuendesha vyuo vya ufundi stadi vipatavyo 27 na chuo kimoja cha ualimu wa
ufundi stad kilichopo manispaa ya mji wa Morogoro.
Alisema
Mamlaka ina vyuo vya ufundi stadi vyenye hadhi vya mikoa katika mikoa
yote Tanzania bara isipokuwa mikoa mipya ya Simiyu, Geita na Njombe huku Rukwa
ikikosa chuo cha Mkoa baada ya chuo chake cha Mpanda kuwa kwenye mpaka wa Mkoa
mpya wa Katavi.
Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa Geita
Magalula Said aliipongeza mamlaka hiyo huku akiahidi kuwa mkoa wa Geita
utashirikiana nao kikamilifu, ili kupanua wigo wa kuwawezesha vijana wengi
kupata elimu na mafunzo ya ufundi stadi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment