Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani), moja kati ya mashine 4 za kurudufu CD feki zilizokamatwa katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa wa Polisi, D/SSGT Daniel Gingo. |
KAMPUNI
ya Udalali ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi
wake Alex Msama ikishirikiana na Jeshi la Polisi Kituo cha Urafiki na Wizara ya
Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, imekamata kompyuta za kufyatua kazi feki
za wasanii zenye thamani ya mil18.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama,
alisema mitambo hiyo imekamatwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya pande hizo tatu
pamoja na sapoti ya wasamaria wema. Alisema kopyuta, mashine na kazi feki zenye
thamani ya mamilioni ya fedha, zimekamatwa eneo la Kimara-Machungwani, jijini
Dar es Salaam na mtuhumiwa huyo amefikishwa katika kituo cha Polisi kwa ajili
ya mchakato wa kiheria wa kufikishwa mahakamani.
Msama
alisema akiwa mdau wa masuala ya burudani kupitia kampuni yake ya Msama
Promotions Ltd ambayo imekuwa ikiratibu matamasha ya Muziki wa Injili, amekuwa
akiguswa na kitendo wanjanja wachache kunufaika na jasho la kazi ya
wengine.Alisema wizi wa kazi za wasanii mbalimbali umekuwa kikwazo cha
mafanikio ya wahusika ambao licha ya kuifanya kazi hiyo kwa muda mrefu,
wameshindwa kupiga hatua kiuchumi kutokana na wajanja hao kuingiza kazi feki
mtaani ambazo huuzwa kwa bei ya kutupa.
Msama
alisema kazi hiyo ngumu ambayo imekuwa ikifanywa na kampuni yake kwa
kushirikiana na wadau wengine, anashukuru kwamba kadiri siku zinavyosogea wengi
wamezidi kukamatwa kutokana na ushirikiano ambao wamekuwa wakipewa.“Msama
Auction Mart tunachukua nafasi hii kulipongeza Jeshi la Polisi hasa Kituo cha
Ubungo ambacho wamekuwa msaada mkubwa kwetu katika vita hii ya kupambana na
wezi wa
kazi za wasanii,” alisema Msama.
Aliongeza,
kwa ushirikiano mkubwa wa Jeshi la Polisi na Wizara ya Habari, Utamaduni,
Vijana na Michezo, anashukuru kazi hiyo imekuwa ikisonga mbele kwa kazi feki
kuzidi kukamatwa katika maeneo mbalimbali ya nchi katika kulinda maslahi ya
wasanii.Alisema tangu kuanza kwa kazi hiyo ngumu ya kukabiliana na wizi wa kazi
za wasanii, kampuni yake imekamata vifaa mbalimbali vya kukamilisha kazi hiyo
na kazi zenye jumla
ya
shilingi bil.12.
Msama
alisema kampuni yake imejitwika jukumu hilo zito kwa lengo la kuona wasanii wa
Tanzania wananufaika na ubora wa kazi zao katika kuendesha maisha yao kwamba
kupitia vipaji vyao, wahusika waweze kujiajiri.Alisema, katika mazingira ya
sasa ambapo jasho la wasanii linaishia mikononi mwa wajanja wachache ambao
wamekuwa wakichakachua kazi, kamwe wasani hawawezi kupata kipato cha kutosha
kuboresha maisha yao.
Msama
ametoa wito pia kwa wasamaria wema sio tu kutoa taarifa kwa kampuni yake au
Jeshi la Polisi za kuwafichua wanaojihusisha na uchakachuaji wa kazi za
wasanii, pia kuacha kununua kazi feki japo huuzwa kwa bei ya
kutupa.Baadhi ya wananchi walioshuhudia baadhi ya vifaa na kazi feki, kwa
nyakati tofauti wameipongeza kampuni ya Msama Auction Mart kwa kazi hiyo ngumu
kwa maslahi
ya
wasanii.
Kelvin
Living na Iddy Abbas wa Mabibo, kwa nyakati tofauti, wameomba kazi hiyo iwe
endelevu kwa sababu wajanja hao wachache wanachangia wasanii kukosa maslahi
mazuri kupitia vipaji vyao.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment