Hatma ya rapper Chidi Benz kuhusiana
na kama ataachiwa huru au kufungwa jela kutokana na mashtaka matatu
yanayomkabili kufuatia kukamatwa na madawa ya kulevya, haikuweza kujulikana
Alhamis hii baada ya kupanda tena kizimbani kwenye mahakama ya Kisutu jijini
Dar es Salaam.
Chidi amepangwa kurejea tena
mahakamani hapo January 15, 2015. Juzi rapper huyo alikuwa na imani kuwa
Alhamis hii angeweza kujua hatma yake na pia kuwaomba watu wamkumbuke kwenye
sala.
“Kesho (jana) ni judgement yangu na
ni mwisho wa kesi yangu pale kwa hakimu mkazi Kisutu,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Najua nimekosea lakini sio sana
kuliko makosa yote,muhimu ni kusamehe na kuondoa hasira na mimi,msipoteze Imani
na mimi,nimekua msanii mzuri na bora kwa kipindi choote..nikiwa kazini
inafahamika nachokifanya,sijawai kosea kuifanya kazi yangu hayo mengine ni
mengine tayari..mnaweza kutokea kwa Sapot na naomba Mniombee.nisirudi kule.Tafadhar.”Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment