Polisi mkoani Pwani limelazimika kuingilia kati kutuliza kuzuka kwa mapigano kati ya wafugaji wa jamii ya Wasukuma na Wamang’ati baada ya kutokea mauaji ya watu wawili chanzo kikiwa ni kuibwa kwa ng’ombe 51
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Pwani Ulrich Matei amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi
katika eneo la Kitale tarafa ya Chole wilayani Kisarawe ambapo watu wawili
wameripotiwa kufariki dunia katika tukio hilo.
Mkuu wa
wilaya ya Kisarawe Fatuma Kimario amethibitisha kutokea kwa mauaji ya watu
wawili yaliyosababishwa na tukio la wizi wa ng’ombe uliofanywa na kijana wa
Kimang’ati.
Aidha Bi
Kimario amesema kuwa katika tukio hilo watuhumiwa wanne wanaendelea kuhojiwa na
vyombo vya dola huku pikipiki nane zikiwa zimekamatwa baada ya kuachwa na
maedereva waliokuwa wakiziendesha .
Sanjari
na hayo bi. Kimario amesema kuwa hali ni shwari eneo la tukio na vyombo vya
ulinzi na usalama vimetoka eneo la tukio na amelaani kitendo cha wafugaji
kujichukulia sheria mkononi baada ya kumkamata na kumuua mtuhumiwa anayedaiwa
kuiba ng’ombe hizo na pia upande wa pili kuamua kulipiza kisasi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment